Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchina inahimiza nchi tajiri kutimiza haraka ahadi za kupunguza utoaji wa gesi joto na haribifu kwenye anga

Uchina inahimiza nchi tajiri kutimiza haraka ahadi za kupunguza utoaji wa gesi joto na haribifu kwenye anga

Kwa upande mwengine, mjumbe wa Uchina, alitoa mwito maalumu kwa zile nchi zenye maendeleo ya viwanda, unaozihimiza kutimiza, kwa uaminifu, ahadi walizotoa siku za nyuma na kuongoza kwenye kadhi ya kupunguza utoaji wa hewa chafu kwenye anga, kwa viwango vilivyo vikubwa,

na vile vile kuzitaka nchi masikini zipatiwe misaada ya fedha na teknolojiya ya kisasa, itakayoziwezesha kukabliana na matatizo yanayoletwa na mababdiliko ya hali ya hewa duniani. Jiang Yu, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uchina, aliyasema hayo wakati akijibu suala kuhusu Mkutano wa Copenhagen, kwenye mahojiano ya kila wiki aliokuwa nayo na waandishi habari. Jiang alisisitiza Uchina itaendelea kuchukua hatua za utendaji na msimamo utakaosaidia kuleta mafanikio ya kuridhisha, kwenye Mkutano wa Copenhagen.