Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UM kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ahimiza wapatanishi kuandaa kidharura marekibisho ya kifedha na kitaaluma kumudu bora athari za gesi chafuzi

Mkuu wa UM kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa, ahimiza wapatanishi kuandaa kidharura marekibisho ya kifedha na kitaaluma kumudu bora athari za gesi chafuzi

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM ya Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) kwenye mahojiano aliofanya Ijumanne na waandishi habari, alisema ufunguzi wa Mkutano Mkuu ulianza kwa "hatua ya kutia moyo, na katika nafasi muafaka,

ambapo wawakilishi wa kimataifa walishuhudiwa kupiga mbiu ya kuhimiza kuchukuliwa hatua za dharura ili kukamilisha mapatano yao," mwelekeo unaohitajika kutekelezwa haraka na Mataifa Wanachama. De Boer alishinikiza kwamba Mkutano wa Copenhagen unawajibika kukamilisha "kwa vitendo halisi, ahadi za kauli" kabla ya vikao kuhitimishwa. Kwa kuambatana na mwelekeo kama huu, aliongeza kusema de Boer, "Mkutano wa Copenhagen una matarajio ya kuwasilisha mageuzi yanayofaa yatakayochochea vitendo halisi, vitakavyohamasisha mataifa kutekeleza mabadiliko muhimu kwenye udhibiti wa gesi chafuzi zinazoathiri hali ya hewa." Alionya kwamba walimwengu hauna tena muda wa kupoteza kwenye utekelezaji wa miradi ya kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa, hasa katika mataifa yanayoendelea.