Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Alkhamisi Baraza la Usalama lilisikilia taarifa ya faragha, iliowasilishwa kwenye ukumbia wa majadiliano, na Haile Menkerios, KM Msaidizi Juu ya Masuala ya Kisiasa, kuhusu shambulio la bomu la kujitoa mhanga liliofanyika asubuhi kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu. Baada ya hapo, Baraza liliitisha kikao rasmi cha hadhara ambacho kilipitisha azimio la Maelezo ya Raisi (Presidential Statement), taarifa iliolaani shambulio la kigaidi kwa kauli kali kabisa, na kusisitiza kufanyike uchunguzi kamili kuhusu tukio hilo na kutaka wakosaji wote washikwe na kupelekwa mahakamani, haraka iwezekanavyo. Baraza la Usalama limetilia mkazo ya kuwa litaendelea kuunga mkono umma wa Usomali na Serikali ya Mpito, utawala ambao Mawaziri wake watatu walikuwa miongoni mwa watu waliouawa na shambulio la bomu la mhanga.

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), asubuhi Ijumaa aliwakilisha ripoti mpya kuelezea kazi zinazoambatana na suala la Darfur. Alisema mnamo miezi ya karibuni, juhudi zote kuhusu suala la Darfur "zilishuhudiwa kuishinikiza Sudan kuhishimu majukumu yake kama ni Taifa Mwanachama wa UM, kwa kusitisha vitendo vya uhalifu na kuwakamata wale watu walioshitakiwa na Mahakama ya ICC." Alisema kwamba Raisi Omar al-Bashir, mmoja ya watuhumiwa wa Mahakama, yeye alinyimwa uhuru wa kusafiri kwenye yale Mataifa ambayo angeliweza kushikwa angelizuru huko. Aliongeza kusema taratibu za kuwadharau wakosa walioshitakiwa na Mahakama ni tabia yenye kuonyesha "mwelekeo wa dhamana ya mwisho kwenye utekelezaji wa hati za kuwakamata watuhumiwa husika." Wakati huo huo, Mwendesha Mashitaka Moreno-Ocampo alihadharisha kwamba anahitajia kuungwa mkono kikamilifu na Baraza la Usalama ili kuhakikisha uangalizi wa Baraza la Usalama unabakia kuhusu haja ya kuwatia mbaroni watuhumiwa kusitisha makosa ya jinai yanayodaiwa kutukia katika Darfur.

Catherine Bragg, KM Msaidizi kwa Masuala ya Kiutu, na ambaye pia ni Naibu Mratibu wa UM katika Kufarajia Misaada ya Dharura anatarajiwa Ijumatatu ya tarehe 07 Disemba (2009), kuanza ziara ya siku tatu katika Zimbabwe. Ripoti za Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) zilieleza makusudio ya ziara hasa ilikuwa ni kufanya mapitio ya mazingira ya kiutu ndani ya nchi, ili kupata taarifa za jumla juu ya fungamano baina ya shughuli za kuhudumia misaada ya kiutu na juhudi za mapema za mashirika ya UM na mashirika wenzi, katika kufufua huduma za pamoja, ili kukidhi mahitaji ya umma. Bragg atakutana na maofisa wa Serikali na wahudumia misaada ya kiutu na kushauriana nao hatua za kuchukuliwa kuitika mapema maombi ya kufadhilia misaada ya kiutu Zimbabwe. Anatarajiwa kuzuru vile vile baadhi ya miradi ya kiutu na kujionea binafsi namna mipango hii inavyotekelezwa, na baadaye atakutana na jamii ya wafadhili wa kimataifa waliopo kwenye eneo. Bragg anatazamiwa kuanzisha kampeni ya kuchangisha Mfuko wa Jumla (CAP) kuisaidia Zimbabwe kihali kwa 2010.

Kwa sababu ya kuharibika, kwa kasi, kwa afya ya mwanaharakati wa haki za binadamu wa kutoka Laayoune, Sahara ya Magharibi, anayeitwa Aminatou Haidar, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, António Guterres, ameziomba serikali mbili husika za Uspeni na Morocco, kuzingatia utaratibu wa kufikia maafikiano juu ya tatizo la kiutu linalohatarisha maisha ya Bi Haidar. Mwanaharakati huyu ameahidi kuwa ataendeleza mgomo wa muda mrefu wa kukaa na njaa kwenye eneo alipo mpaka pale mahitaji yake ya kurejeshwa kwao yatakapokamilishwa. Kamishna Mkuu wa UNHCR ameeleza kwamba ametoa mwito wa kumsaidia Bi Haidar kwa sababu ya huruma ya kiutu. Aminatou Haider alianza kufunga mnamo tarehe 16 Novemba (2009), baada ya Morocco, kumfukuza nchini kutoka Sahara Magharibi, na akaamua wakati wote huu, kuegesha maskani kwenye kiwanja cha ndege cha Lanzarote, katika Visiwa vya Canary, vinavyomilkiwa na Uspeni, akisubiri kurudishwa kwao Sahara ya Magharibi.

Alkhamisi Baraza la Usalama lilisikilia taarifa ya faragha, iliowasilishwa kwenye ukumbia wa majadiliano, na Haile Menkerios, KM Msaidizi Juu ya Masuala ya Kisiasa, kuhusu shambulio la bomu la kujitoa mhanga liliofanyika asubuhi kwenye mji mkuu wa Usomali wa Mogadishu. Baada ya hapo, Baraza liliitisha kikao rasmi cha hadhara ambacho kilipitisha azimio la Maelezo ya Raisi (Presidential Statement), taarifa iliolaani shambulio la kigaidi kwa kauli kali kabisa, na kusisitiza kufanyike uchunguzi kamili kuhusu tukio hilo na kutaka wakosaji wote washikwe na kupelekwa mahakamani, haraka iwezekanavyo. Baraza la Usalama limetilia mkazo ya kuwa litaendelea kuunga mkono umma wa Usomali na Serikali ya Mpito, utawala ambao Mawaziri wake watatu walikuwa miongoni mwa watu waliouawa na shambulio la bomu la mhanga.

Luis Moreno-Ocampo, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC), asubuhi Ijumaa aliwakilisha ripoti mpya kuelezea kazi zinazoambatana na suala la Darfur. Alisema mnamo miezi ya karibuni, juhudi zote kuhusu suala la Darfur "zilishuhudiwa kuishinikiza Sudan kuhishimu majukumu yake kama ni Taifa Mwanachama wa UM, kwa kusitisha vitendo vya uhalifu na kuwakamata wale watu walioshitakiwa na Mahakama ya ICC." Alisema kwamba Raisi Omar al-Bashir, mmoja ya watuhumiwa wa Mahakama, yeye alinyimwa uhuru wa kusafiri kwenye yale Mataifa ambayo angeliweza kushikwa angelizuru huko. Aliongeza kusema taratibu za kuwadharau wakosa walioshitakiwa na Mahakama ni tabia yenye kuonyesha "mwelekeo wa dhamana ya mwisho kwenye utekelezaji wa hati za kuwakamata watuhumiwa husika." Wakati huo huo, Mwendesha Mashitaka Moreno-Ocampo alihadharisha kwamba anahitajia kuungwa mkono kikamilifu na Baraza la Usalama ili kuhakikisha uangalizi wa Baraza la Usalama unabakia kuhusu haja ya kuwatia mbaroni watuhumiwa kusitisha makosa ya jinai yanayodaiwa kutukia katika Darfur.

Catherine Bragg, KM Msaidizi kwa Masuala ya Kiutu, na ambaye pia ni Naibu Mratibu wa UM katika Kufarajia Misaada ya Dharura anatarajiwa Ijumatatu ya tarehe 07 Disemba (2009), kuanza ziara ya siku tatu katika Zimbabwe. Ripoti za Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) zilieleza makusudio ya ziara hasa ilikuwa ni kufanya mapitio ya mazingira ya kiutu ndani ya nchi, ili kupata taarifa za jumla juu ya fungamano baina ya shughuli za kuhudumia misaada ya kiutu na juhudi za mapema za mashirika ya UM na mashirika wenzi, katika kufufua huduma za pamoja, ili kukidhi mahitaji ya umma. Bragg atakutana na maofisa wa Serikali na wahudumia misaada ya kiutu na kushauriana nao hatua za kuchukuliwa kuitika mapema maombi ya kufadhilia misaada ya kiutu Zimbabwe. Anatarajiwa kuzuru vile vile baadhi ya miradi ya kiutu na kujionea binafsi namna mipango hii inavyotekelezwa, na baadaye atakutana na jamii ya wafadhili wa kimataifa waliopo kwenye eneo. Bragg anatazamiwa kuanzisha kampeni ya kuchangisha Mfuko wa Jumla (CAP) kuisaidia Zimbabwe kihali kwa 2010.

Kwa sababu ya kuharibika, kwa kasi, kwa afya ya mwanaharakati anayegombania haki za binadamu wa kutoka Laayoune, Sahara ya Magharibi, anayeitwa Aminatou Haidar, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji, António Guterres, ameziomba serikali mbili husika za Uspeni na Morocco, kuzingatia utaratibu wa kufikia maafikiano juu ya tatizo la kiutu linalohatarisha maisha ya Bi Haidar. Mwanaharakati huyu ameahidi kuwa ataendeleza mgomo wa muda mrefu wa kukaa na njaa kwenye eneo alipo mpaka pale mahitaji yake ya kurejeshwa kwao yatakapokamilishwa. Kamishna Mkuu wa UNHCR ameeleza kwamba ametoa mwito wa kumsaidia Bi Haidar kwa sababu ya huruma ya kiutu. Aminatou Haider alianza kufunga mnamo tarehe 16 Novemba (2009), baada ya Morocco, kumfukuza nchini kutoka Sahara Magharibi, na akaamua wakati wote huu, kuegesha maskani kwenye kiwanja cha ndege cha Lanzarote, katika Visiwa vya Canary, vinavyomilkiwa na Uspeni, akisubiri kurudishwa kwao Sahara ya Magharibi.