2 Disemba 2009
Alkhamisi KM anatazamiwa kumteua msanii maarufi wa Marekani, Stevie Wonder kuwa Mjumbe wa Amani wa UM atakayejihusisha zaidi na huduma za kusaidia walemavu kote ulimwenguni.
Stevie Wonder ni maarufu katika ufadhili wa umma muhitaji, kwa kupitia Kamati ya Raisi wa Marekani juu ya Ajira ya Walemavu, Taasisi ya Watoto Wanaogua Kisukari na pia Shirika la Vijana Walio Vipofu wa Marekani. Atajiunga na orodha ya Wafadhili wa Amani 10 wengineo wenye kutetea shughuli za UM katika ulimwengu, kwa natija za umma wote wa kimataifa.