Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majadiliano ya kibiashara yanahitaji kuzingatia kidhati tatitzo sugu la njaa, asihi mtetezi wa haki ya chakula

Majadiliano ya kibiashara yanahitaji kuzingatia kidhati tatitzo sugu la njaa, asihi mtetezi wa haki ya chakula

Profesa Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu wa UM anayetetea haki za mtu kupata chakula, amepongeza taarifa za wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO),

iliotolewa Geneva na nchi zenye maendeleo ya viwanda pamoja na zile zenye maendeleo haba, ambazo zilitambua umuhimu mkubwa wa kudhaminia akiba maridhawa ya chakula duniani, kwa kuingiza masuala yanayohusu chakula kwa wote kwenye mifumo ya biashara ya wahusika wengi. Alikumbusha kwamba kauli hizi zinatia moyo, lakini kwa walimwengu kuwa na imani nazo kidhati, "serikali zinazojadiliana masuala ya kibiashara zitahitajika kuwa na msimamo usio wa kigeugeu, wenye kulingana na muafaka mpya wa kimataifa juu ya utatuzi wa janga la njaa ulimwenguni." Profesa De Schutter aliyasema haya wakati Shirika la WTO linafanyisha kikao cha mawaziri mjini Geneva, na kusailia mada ya kudhibiti bora akiba ya chakula duniani, kwa sababu anaamini mfumo uliopo sasa hivi juu ya biashara ya wahusika wengi, unahitajia marekibisho makubwa ya haraka, yatakayoleta natija zaidi kwa nchi maskini.