Msemaji wa awali wa Ban Ki-moon astaafu na kuhishimiwa na UM
Msemaji wa awali wa KM Ban Ki-moon, yaani Michèle Montas, amestaafu rasmi kuanzia Ijumatatu, tarehe 30 Novemba.
Kwenye kikao cha kila siku cha adhuhuri cha UM na waandishi habari wa kimataifa, kinachofanyika Makao Makuu, KM Ban Ki-moon alihudhuria mkusanyiko huo, kumwaga Msemaji wake, ambapo alitoa shukrani zake. Alisema KM kwamba mnamo miaka mitatu iliopita, alipata fursa ya kufanya kazi, takriban kila siku, na kwa furaha kuu, na Michèle Montas ambaye alisisitiza alikuwa ni "Msemaji shupavu wa UM, mtaalamu aliyebobea kitaaluma, aliyejitolea kikazi na aliye mtu mwema kabisa." Alikumbusha kwamba Michèle Montas ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo aliyemteua kufanya kazi naye baada ya yeye kuchaguliwa kuwa KM, kwa sababu alisema Michèle alikuwa "ni mtu mmoja aliyejumuisha maadili ya kiwango cha juu kuhusu uadilifu wa binafsi na uaminifu wa uandishi habari." Aliongeza kusema, Michèle ni "mtu aliye thabiti, mstahamilivu, na vile vile karimu .. na aliyeshwari na tulivu." KM alisema kustaafu kwa Msemaji wake huyu humaanisha kutakuwepo pengo lisiokuwa rahisi kulifuatilia, kwa sababu Michèle Montas alikuwa ni Msemaji mwenye kuonyesha "hishima kuu kila anapokabiliwa na vimondo vya mashambulio ya kikazi kutoka waandishi habari."