Skip to main content

OCHA inahadharisha, Chad Mashariki yatota kwenye hali ya wasiwasi

OCHA inahadharisha, Chad Mashariki yatota kwenye hali ya wasiwasi

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kwamba hali katika eneo la Chad Mashariki inaendelea kuzongwa na ukosefu wa usalama na wasiwasi, ulioselelea kwenye eneo katika kipindi cha karibuni, mazingira ambayo yanazorotisha shughuli za kukidhia mahitaji ya kiutu kwa waathirika wa hali ya msukosuko na vurugu.

OCHA inasema tatizo la kuteka nyara wahudumia misaada ya kiutu ni kipengele kipya kinachoathiri zaidi shughuli za kiutu kwenye maeneo yaliopambwa na vitendo vya ujambazi katika Chad mashariki, na hata kwenye jimbo la magharaibi la Sudan la Darfur na kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati. UM unaashiria watu wanaokadiriwa 96,000, wanaohitajia misaada ya kiutu kidharura, sasa hivi wanakabiliwa na hatari ya kutota, na kutotoma, kihali, pindi mashirika yanayohudmia misaada ya kiutu yatalazimika kupunguza operesheni zao kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Serikali ya Chad imetangaza kuwa itachukua hatua kadha za kuimarisha hifadhi bora kwa raia na wahudumia misaada ya kiutu wa kimataifa kwa kuwapatia ulinzi wa polisi.