Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za Ijumatatu kwenye Baraza la Usalama

Harakati za Ijumatatu kwenye Baraza la Usalama

Baraza la Usalama asubuhi lilisikiliza ripoti kutoka Edmond Mulet, KM Msaidizi kuhusu Operesheni za Ulinzi Amani za UM juu ya Darfur, ambaye alisisitiza hali ya usalama katike eneo bado ni ya kuregarega.

Alihadharisha ya kuwa Vikosi vya Pamoja vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) vinaendelea kukabiliwa na matatizo ya kutoweza kwenda watakapo kuendeleza shughuli zao, suala ambalo UM utajitahidi kushauriana na Serikali ya Sudan ili kulitatua kipamoja, na kwa ridhaa ya wote. Ama kuhusu mpango wa amani kwa Darfur, Mulet alisema katika miezi ijayo kutahitajika kufanyika maendeleo makubwa kwenye mazungumzo yanayoambatana na masuala ya kugawana madaraka, utajiri wa eneo, maamirisho ya usalama pamoja na fidia ya malipo kwa wahusika wote, pindi UM umewania, kidhati, kuhakikisha uchaguzi utafanyika kama inavyotakiwa na kuwa na maana inayoridhisha, kwa wakazi wote wa Darfur. Kabla ya kusailia Darfur, Baraza la Usalama lilipitisha maazimio mawili - azimio la awali, liliongeza muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya JKK mpaka Novemba 30, 2010, na vile vile kupendekeza muda wa kamati ya Kundi la Wataalamu juu ya JKK, nao pia uongezwe, kwa kipindi hicho hicho. Azimio la pili la Baraza la Usalama limeongeza kwa miezi kumi na mbili ziada, madaraka yaliofadhiliwa nayo Mataifa Wanachama na mashirika ya kikanda na kuyahimiza yalioruhusiwa kujiunganisha kikamilifu na shughuli za Serikali ya Mpito ya Usomali kwenye zile shughuli na harakati za kupiga vita uharamia na ujambazai unaofanyika kwenye mwambao wa Usomali. Vile vile, kuanzia Ijumanne, tarehe mosi Disemba, Uraisi wa Baraza la Usalama utaoongozwa na Burkina Faso, kwa kulingana na kanuni za Uraisi wa Duru wa Baraza.