Upigaji marufuku minara ya misikiti Uswiss ni kitendo cha ubaguzi dhidi ya WaIslam, asisitiza mtaalamu wa UM wa haki za binadamu

Upigaji marufuku minara ya misikiti Uswiss ni kitendo cha ubaguzi dhidi ya WaIslam, asisitiza mtaalamu wa UM wa haki za binadamu

Asma Jahangir, Mkariri (Mtetezi) Maalumu juu ya uhuru wa kiitikadi na haki ya kufuata dini, ametoa taarifa kwa waandishi habari, kufuatia kura ya maoni iliofanyika Uswiss, ya kupiga marufuku ujenzi wa minara mipya ya misikiti nchini humo, taarifa iliosisitiza kwamba marufuku hayo huwa yanabagua kidhahiri jamii ya WaIslam waliopo katika Uswiss.

Bi. Jahangir alisema ana "wahaka mkuu kuhusu madhara yatakayozuka siku za baadaye, kutokana na kura ya maoni ya kuweka vikwazo vya kidini viliopita kiasi, vyenye kubagua kidhahiri jumuiya ya WaIslam wa Uswiss", vikwazo ambavyo, alisema, Kamati ya UM dhidi Haki za Binadamu ilisisitiza mwezi uliopita, vinakwenda kinyume na majukumu ya Uswiss chini ya sheria za kimataifa juu ya haki za binadamu.