Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa Falastina

Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa Falastina

Tarehe 29 Novemba huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa KiFalastina.

Ilivyokuwa siku hiyo imeangukia Ijumapili, taadhima zake zinafanyika, leo Ijumatatu, hapa Makao Makuu. Kwenye risala ya KM Ban Ki-moon kuihishimu Siku ya Ushikamano na Umma wa KiFalastina alibainisha wasiwasi alionao juu ya kuzorota kwa, karibu mwaka mmoja, yale mazungumzo ya amani kati ya Israel na WaFalastina. KM ametilia mkazo umuhimu wa kuandaa mazingira yanayoridhisha yatakayoziwezesha pande zote mbili husika na mzozo wa Mashariki ya Kati, kurejea kwenye meza ya majadiliano. KM amesisitiza kwamba, kwa amani kudumu kwenye eneo, ni lazima kuhakikisha kunakuwepo kwa mamlaka huru, ya Taifa la Falastina.