Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Awali)

Mazungumzo kuhusu Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto (Sehemu ya Awali)

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) majuzi lilichapisha ripoti muhimu yenye mada isemayo "Hali ya Watoto Duniani kwa 2009".

Ripoti iliangaza zaidi kwenye mchango wa Mataifa Wanachama katika utekelezaji wao wa Mkataba wa Haki za Mtoto. Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Ann Veneman alisema Mkataba wa Haki za Mtoto ulifanikiwa kurekibisha hisia ya kimataifa na kuzisaidia serikali, na umma kwa ujumla, kuelewa uzuri zaidi mahitaji halisi ya watoto na haki zao ulimwenguni. Kwa mujibu wa ripoti, kuanzia miaka 20 iliopita hadi hivi sasa maendeleo makubwa kadha yalipatikana kwenye uetekelezaji wa haki za watoto; kwa mfano, vifo vya watoto vilionekana kupungua kwa kiwango cha kutia moyo katika maeneo mbalimbali ya dunia. Vile vile idadi kubwa ya watoto walirajisiwa kuhudhuria skuli za msingi, au skuli za pramiari, katika kipindi cha miaka 20 iliopita. Kadhalika, mafanikio kadha mengineyo yalishuhudiwa katika miaka ya karibuni, kwenye utekelezaji wa haki za mtoto.

Mnamo tarehe 20 Novemba, 2009 kulifanyika tafrija maalumu hapa kwenye Makao Makuu, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 tangu Mkataba juu ya Haki za Mtoto uliporidhiwa na kuidhinishwa kimataifa. Watoto kutoka nchi mbalimbali za dunia walikusanyika kwenye Makao Makuu, ikijumlisha watoto kutoka Afrika Mashariki.

Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM imetarayarisha makala mbili zinazoambatana na taadhima za kutimia miaka 20 kwa Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto. Sehemu ya awali inajumlisha mahojiano aliokuwa nayo mwendeshaji vipindi AZR na binti Millicent Atieno Odondo kutoka Kenya, ambaye alikuwa miongoni mwa vijana waliohudhuria taadhima za KM.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.