Skip to main content

WFP imetangaza marekibisho ya kuhudumia pekee eneo la Kaskazini-Magharibi la JKK na katika Jamhuri ya Kongo

WFP imetangaza marekibisho ya kuhudumia pekee eneo la Kaskazini-Magharibi la JKK na katika Jamhuri ya Kongo

Shirika la UM juu Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kwamba litarekibisha huduma zake katika JKK na taifa jirani la Jamhuri ya Kongo.

WFP imeleza hivi sasa inajitayarisha kuhudumia chakula makumi maelfu ya raia wa Kongo waliolazimika kuhama makwao kutokana na uhasama na miripuko ya mapigano katika jimbo la Equateur katika JKK na katika kijiji cha Dongo. Watu 38,000 waliripotiwa kukimbia mapigano makali yaliopamba mwezi uliopita katika JKK na kuvuka mto kumiminikia taifa jirani la Jamhuri ya Kongo. Kadhalika, raia 14,000 wamesajiliwa kwa sasa hivi kuwa wahamiaji wa ndani katika JKK na wanategemea misaada ya kihali kutoka mashirika ya kimataifa. Tathmini ya UM imethibitisha kuwepo dharura kubwa ya chakula kwenye sehemu zote mbili za mto, hasa kwa wanawake na watoto wadogo, ambao kwa muda wa wiki chache sasa wamo mbioni wakitangatanga kutafuta nusura ya maisha. WFP hivi sasa inatathminia hali halisi kwenye sehemu za Dongo, na inajitayarisha pia kuanzisha miradi maalumu ya kugawa chakula mnamo wiki ya pili ya Disemba kutoka akiba iliohifadhiwa nchini.