UM imethibitisha mabaki ya mtumishi wa UM aliyepotea miaka mingi Lebanon

24 Novemba 2009

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon amearifiwa kupatikana kwa mabaki ya Alec Collett katika Lebanon mashariki.

Marehemu Collett alikuwa mtumishi aliyefanya kazi na Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA), na alipotea Lebanon katika 1985. KM aliwashukuru wenye madaraka katika Uingereza na Lebanon ambao, kwa miaka mingi, walijishughulisha na juhudi za kulitatua suala hili lakupotea kwa Colett. Vile vile KM alipongeza kazi ya Idara ya UM juu ya Ulinzi na Usalama wa Wafanyakazi (DSS) kwenye uchunguzi wa kutambua kiini hasa cha yaliomfika Collett. KM alisema ijapokuwa alisikitishwa na kifo cha Alec Collett, alitumai kupatikana kwa mabaki yake itajumlisha hatua itakayosaidia kuwatuliaza aila yake, na aliahidi UM utawapatia msaada wote unaohitajika, katika siku za baadaye, kuhitimisha msiba wao.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter