Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Haki za Mtoto wakamilisha miaka ishirini

Mkataba wa Haki za Mtoto wakamilisha miaka ishirini

Tarehe ya leo, Novemba 20, 2009 inawakilisha kumbukumbu ya maiaka 20 ya Mkataba juu ya Haki za Mtoto.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Mtoto (UNICEF) limekariibisha tangazo la Serikali ya Mpito ya Usomali kwamba imedhamiria kurihdia na kuuidhinisha Mkataba wa Kimataifa juu ya Haki za Mtoto. Usomali ilikuwa ni moja ya mataifa mawili yaliosalia duniani yaliotia sahihi Mkataba bila ya kuuidhinisha. Kwa Serikali ya Usomali kukubali kuidhinisha Mkataba inamaanisha umhimu unaopewa na wenye mamlaka juu ya haki za watoto katika eneo ambalo limezama kwenye vurugu, ufukara sugu na utapiamlo uliokiuka ada.