Skip to main content

Bodi la Uchunguzi juu ya ukiukaji wa haki za binadamu Guinea laanza kazi

Bodi la Uchunguzi juu ya ukiukaji wa haki za binadamu Guinea laanza kazi

Makamishna wa tume ya KM wanajumlisha Mohamed Bedjaoui, Françoise Ngendahayo Kayiramirwa na Pramila Patten ambao wanatazamiwa kuendeleza uchunguzi huru kutathminia ukweli, na kutoa mapendekezo yao juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya wale waliowajibika na msiba dhidi ya raia uliotukia Guinea mwezi Septemba. Wajumbe wa tume watazuru Guinea kuendeleza kazi zao kuanzia tarehe 25 Novemba mpaka tarehe 04 Disemba mwaka huu.