ICTR imeamrisha kuachiwa kutoka vizuizini wafungwa wawili

18 Novemba 2009

Mahakama ya Kimataifa juu ya Rwanda (ICTR) imeamua kumwachia huru Hormisdas Nsengimana, aliyekuwa padri wa Rwanda, baada ya kuonekana hana hatia juu ya mashitaka ya kushiriki kwenye vitendo vya mauaji ya halaiki na makosa ya jinai dhidi ya utu na kuamrisha afunguliwe haraka kutoka Kituo cha UM cha Kuwekea Watu Kizuizini kiliopo Arusha, Tanzania.

Kadhalika Ijumatatu, Korti ya Rufaa ya Mahakama juu ya Rwanda iliamuru kuachiwa huru, kutoka kizuizini, kwa haraka, Protais Zigiranyirazo, shemeji wa aliyekuwa Raisi wa Rwanda, ambaye siku za nyuma alishtakiwa makosa ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Korti ya Rufaa ilibadilisha makosa ya nyuma, yaliomtia hatiani Zigiranyirazo baada ya kugundua makosa ya kisheria kadha na vile vile baada ya kufichua dosari katika ushahidi uliotolewa, kwa uwiano na tathmini ya Mahakama ya Kusikiliza Mashtaka baada ya Rufaa, hasa juu ya ushahidi kwamba mshitakiwa hakuwepo kwenye eneo la tukio wakati kosa linafanyika.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud