Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Alain Le Roy Naibu KM juu ya Operesheni za Ulinzi Amani, akifuatana na Mshauri wa KM juu ya Masuala ya Kijeshi, Jenerali Chikadibia Isaac Obiakor, na Anthony Banbury, KM Msaidizi kwa Huduma za Nje za Mashirika ya Ulinzi Amani ya UM, wiki hii wataelekea Uchina kuhudhuria mkutano maalumu wa kuzingatia operesheni za kulinda amani za UM. Wakati watakapokuwepo Beijing, Le Roy atakutana na wajumbe kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uchina na Wizara ya Mambo ya Nje na kusailia nao mchango wa Uchina katika kuimarisha huduma za kulinda amani ulimwenguni.

Wakati huo huo, Susana Malcora, Naibu KM juu ya Huduma za Nje za Mashirika ya Ulinzi Amani ya UM anazuru Sudan, na yupo Khartoum kwa sasa ambapo Ijumatatu alihudhuria kikao cha saba cha kuzingatia Mfumo wa wa Pande Tatu juu ya Amani kwa Darfur. Naibu KM wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan, Dktr. Mutrif Siddiq, pamoja na Ramtane Lamamra, Kamishna wa Masuala ya Amani wa Umoja wa Afrika (UA) walishiriki kwenye mazungumzo hayo na wakijumuika na Henry Anyidoho, Naibu Mjumbe Maalumu wa Pamoja wa UM-UA kwa Darfur. Wajumbe wote hawa walielezea wasiwasi walionao kuhusu hali ya watumishi mateka wawili wa UNAMID, walioshikwa na kuwekwa vizuizini na makundi yasiotambuliwa, tangu tarehe 29 Agosti 2009. Dktr. Siddiq, kwa upande wake, alirudia tena ahadi ya Serikali ya Sudan iliotilia mkazo umuhimu wa kuwapatia watumishi wote wa UNAMID ulinzi na usalama unaofaa. Kadhalika, kwenye mazungumzo kulizingatiwa masuala yanayohusu matumizi ya helikopta maalumu za vikosi vya wanajeshi wa UNAMID kutoka Ethiopia, ruhusa ya kuanzisha matangazao ya Redio ya UNAMID, usalama wa wafanyakazi, kwa ujumla, na vile vile ugawaji wa maji safi na salama kwa jamii zinazoishi Darfur. Kikao kingine cha Mfumo wa Pande Tatu juu ya Amani kwa Darfur kimeandaliwa kufanyika mwezi Februari 2010 katika mji wa Addis Ababa.

Ijumapili Warsha/Semina Maalumu juu ya Uongozi wa Matumizi ya Intaneti (IGF) ulifunguliwa rasmi katika mji wa Sharm El-Sheikh, na unatarajiwa kuendelea mapaka Ijumatano, kwa lengo la kuzingatia masuala yanayofungamana na faragha ya wanaotumia intanenti, usalama kwa wateja wa mawasiliano ya intaneti na uwazi unaohitajika kuendesha huduma za intaneti bila ya kuharamishwa kisheria. Sha Zukang, Naibu KM wa UM juu ya Masuala ya Kiuchumi na Jamii, alikumbusha kwenye hotuba yake mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho ya kuwa wanatakiwa wachukue uamuzi wa mapema juu ya matumizi halisi ya IGF kwa siku za baadaye, ilivyokuwa sheria zake zinakaribia mwisho wa muda ulioidhinishwa kutumika wa miaka 5, katika 2010. Wahutubu wingi, wakijumlisha maofisa wa kiserikali wa ngazi za juu, wamependekeza kanuni za IGF ziendelee kutumiwa kwa miaka zaidi kupita 2010.

KM leo amewasilisha mbele ya Baraza Kuu ripoti kuhusu fafanuzi za sera zinazoharamisha haki za binadamu za WaFalastina kutokana na vitendo vya Israel kwenye Makao Yaliokaliwa Kimabavu ya WaFalastina. Ndani ya ripoti KM alitoa mwito wenye kuitka Israel kukomesha, haraka, mazingio na vikwazo dhidi ya eneo la Tarafa ya Ghaza; na kuruhusu WaFalastina wa Eneo Liliokaliwa Kimabavu la Ufukwe wa Mto Jordan uhuru halali wa kutembea popote watakapo; na pia kuhakikisha haki za watoto wa KiFalastina zinahishimiwa, ikijumlisha kusimamisha vile vitendo haramu, viliokiuka sheria, vya kukamata na kuwaweka vizuizini watoto wadogo. Aliongeza ya kuwa makundi yote husika yanawajibika kutekeleza, kwa makini zaidi, majukumu yao kwa kulingana na haki za binadamu za kimataifa na sheria za kiutu. Vile vile ripoti ya KM ilipendekeza ujenzi haramu wa ukuta kwenye eneo la Ufukwe wa Magharibi usitishwe haraka, pamoja na ubomoaji haramu wa nyumba za WaFalastina na kuwafukuza makazi.

Tarehe ya leo, 16 Novemba, inaadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuvumiliana. Kwenye risala ya kuiadhimisha siku hii, KM alieleza kwamba uvumilivu wa kitamaduni ni mfumo wa maisha unaotakana na itikadi inayotilia mkazo umuhimu wa imani ya kutuogopa, wala kukhofu tamaduni anuwai za walimwenngu, na kuhimiza umma wa kimataifa kuzipokea kwa moyo mwema tofauti hizo kwa natija za kiutu zitakazonufaisha wote. Vile vile KM alikumbusha UM upo msitari wa mbele katika kuendeleza hali ya kuvumiliana kitamaduni miongoni mwa umma wa kimataifa - ikijumlisha, mathalan, zile shughuli za UM zinazohusika na ulinzi amani kwenye maeneo yenye uhasama, pamoja na kwenye shughuli za kuzuia ugomvi na mapigano, utekelezaji wa mifumo ya kidemokrasia na katika kutekeleza haki za kibinadamu.

Ijumatatu, kwenye mji wa Freetown Mahakama Maalumu juu ya Jinai ya Vita kwa Sierra Leone imeikabidhi Ofisi ya Magereza ya Sierra Leone vituo viwili vya kuweka watu vizuizini, kwenye tafrija ya kihistoria iliowakilisha hitimisho la madaraka ya kazi ya Korti hiyo nchini. Vituo hivi vitatumiwa kuwaweka wafungwa wa kike kuanzia hivi sasa. Mnamo mwezi Agosti 2003, Mahakama Maalumu juu ya Sierra Leone iliwahamisha washitakiwa kwenye vituo vya kushikia watu vya Ofisi ya Magereza ya Sierra Leone na kuyatengeneza upya magereza haya mawili kwa makusudio ya kuwa na mastakimu yanayoridhisha kuweka wanadamu.