WHO yahimiza ugawaji wa mapema wa dawa kinga dhidi ya H1N1
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hadhari maalumu kwa madaktari, inayowasihi kutongojea matokeo ya vipimo vya maabara ya afya kuhusu maambukizi, kabla ya kugawa dawa ya kupambana na virusi vya homa ya mafua ya A/H1N1 kwa wanawake wajawazito wanaodhaniwa wameambukizwa na maradhi hayo.