Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban Ki-moon ahutubia Baraza la Usalama kuzingatia hali katika Afghanistan

KM Ban Ki-moon ahutubia Baraza la Usalama kuzingatia hali katika Afghanistan

Ijumaa alasiri KM Ban Ki-moon alihutubia Baraza la Usalama, kwenye kikao maalumu cha faragha, kuzingatia hali katika Afghanistan.

Alitazamiwa kusailia hali ya usalama na kuwasilisha fafanuzi zake juu ya ziara aliifanya majuzi kwenye mji wa Kabul, Afghanistan kufuatia shambulio la magaidi dhidi ya watumishi wa UM, tukio liliosababisha vifo vya wafanyakazi watano na majeruhi tisa.