Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahadi na maelewano yanahitajika kusukuma mbele majadiliano ya hali ya hewa

Ahadi na maelewano yanahitajika kusukuma mbele majadiliano ya hali ya hewa

Kikao cha mwisho, cha mashauriano, kabla ya mkutano ujao wa Copenhagen (Denmark), kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kimekamilisha mahojiano mjini Barcelona, Uspeni hii leo hii.

Yvo de Boer, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya UM kuhusu Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa (UNFCCC) alitoa mwito maalumu uwenye kuyahimiza Mataifa Wanachama, kuharakisha kufiikia maafikiano ya kimataifa, yenye nguvu, ili kukabiliana vyema na athari haribifu za mabadiliko ya hali ya hewa. Alisema anaamini kikao cha Copenhagen kitawasilisha "kipindi muhimu cha mabadiliko ya kihistoria" hasa ikiwa Mataifa Wanachama "yataahidi kujiwekea masharti, kwa maelewano yatakayoridhisha, kwa ujumla, masilahi ya umma wa kimataifa." Hadi kipindi cha sasa, nchi zenye maendeleo ya viwanda zimeshindwa kuafikiana kiwango cha kuchukuliwa kupunguza hewa chafu inayomwagwa kwenye maeneo yao, na gharama za kuleta marekibisho kwenye uchumi, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.