Skip to main content

UM unasema 'majaribio ya mauaji ya raisi Usomali ni hujma dhidi ya raia wote'

UM unasema 'majaribio ya mauaji ya raisi Usomali ni hujma dhidi ya raia wote'

Majaribio mawili ya karibuni ya kutaka kumwua Raisi wa Usomali, Sharif Sheikh Ahmed yalilaaniwa vikali kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliotolewa na Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah, ambayo aliyafananisha na mashambulio ya mauaji dhidi ya raia wote wa Usomali.

Mjumbe wa KM alisema watu wenye siasa kali Ijumatano walijaribu kumuua tena raisi alipokuwa anarejea Mogadishu kutoka Uganda, ambapo alihudhuria mkutano mkuu wa viongozi wa Afrika. Kitendo hiki kilifuatia majaribio mengine ya maisha ya Raisi wa Usomali yaliofanyika Alkhamisi iliopita, kwenye kiwanja cha ndege cha Mogadishu pale Raisi wa Usomali alipokuwa anapanda ndege kuelekea mkutanoni Kampala. Ould-Abdallah alihadharisha kwamba waasi wenye siasa kali, wanajaribu, kwa mara nyengine tena, kutishia na kuwatia khofu umma wa Usomali ili kuchichea uharibifu ziada kwenye nchi yao. Alisisitiza majaribio ya mauaji yenye kuangamiza raia wasio hatia waliopo mitaani, ikijumlisha wanawake na watoto wadogo, ni utaratibu usiosahihi wa kujinyakulia madaraka; na alikumbusha sheria za kidini zinaharamisha kabisa mauaji ya kujitoa mhanga na hudhoofisha jitihadi zote za kurudisha japo upenu wa utulivu na hali ya kikawaida nchini mwao.