Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM yajitahidi kuhamasisha Mataifa Wanachama, yatakapokutana Copenhagen, kukamilisha mapatano juu ya udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa

UM yajitahidi kuhamasisha Mataifa Wanachama, yatakapokutana Copenhagen, kukamilisha mapatano juu ya udhibiti wa mabadiliko ya hali ya hewa

Janos Pastzor, Mkuu wa Timu ya Ushauri kwa KM juu ya Masuala Yanayohusu Udhibiti wa Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa alinakiliwa akiwaarifu waandishi habari waliokusanyika kwenye mahojiano yaliofanyika Ijumatatu alasiri katika Makao Makuu, kwamba UM una matarajio ya wastani kuhusu uwezekano wa kuwa na mapatano ya sheria ya kulazimisha, kutokana na mkutano mkuu ujao utakaofanyika mwezi Disemba, katika Copenhagen,

na inaaminika itachukua muda mrefu kwa mataifa kuwa na chombo cha sheria ya kutumiwa kipamoja, ili kudhibiti bora uharibifu wa hali ya hewa katika ulimwengu. Hata hivyo alisema KM anaamini msukumo wa kisiasa uliokubaliwa na viongozi wa taifa na serikali 101, waliohudhuria kikao maalumu cha Baraza Kuu, kilichofanyika mwaka huu unawajibika kuimarishwa na kuendelea kulengwa kwenye ile dhamira halisi ya kuwa na mapatano ya kisiasa, yenye sheria ya lazima kutoka mkutano wa Copenhagen, sheria itakayotumiwa kuongoza majadiliano ya siku za baadaye ya kubuni mkataba mpya wa kimataifa kudhibiti bora hali ya hewa na athari zake zinazoletwa na uchafuzi wa mazingira ya kihorera.