Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekaji nyara wa mtumishi wa ICRC Darfur kulaaniwa na ofisa wa UM kwa Sudan

Utekaji nyara wa mtumishi wa ICRC Darfur kulaaniwa na ofisa wa UM kwa Sudan

Mratibu wa UM juu ya Masuala ya Kiutu kwa Sudan, Ameerah Haq amelaani vikali utekwaji nyara wa mtumishi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) anayeitwa Gauthier Lefevre, mwenye uraia wa Kiingereza/Ufaransa, unyakuzi uliofanyika Alkhamisi iliopita, wakati mtumishi huyo alipokuwa anarejea nyumbani kwake Al Geneina, mji mkuu wa jimbo la Darfur Magharibi.

Alisema unyakuzi wa Lefevre "hauleti natija yoyote bali isipokuwa unadhoofisha shughuli za kuhudumia operesheni za kiutu kwa umma muhitaji wa eneo, umma ambao utanyimwa haki ya kupatiwa misaada ya kidharura inayohitajika kunusuru maisha." Aliongeza kusema kosa la jinai ya kuiba watu ni kitendo chenye "kuchafua mazingira ya usalama na utulivu unaotakikana kufarajia vyema misaada ya kiutu, na huathiri vibaya uwezo wa mashirika ya kimataifa kuhudumia chakula na mahitaji ya kimsingi kwenye maeneo yenye shida."