Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuhadharisha, watu milioni sita ziada Ethiopia wanahitajia misaada ya chakula kuwavua na janga la njaa

UM kuhadharisha, watu milioni sita ziada Ethiopia wanahitajia misaada ya chakula kuwavua na janga la njaa

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti Ethiopia imezongwa na mshtuko mkuu wa maafa yenye kuathiri hali ya chakula kwa watu milioni 6 nchini.

Msiba huo unatokana na mchanganyiko wa mvua za kigeugeu, zilizonyesha kwa kiwango kidogo mnamo miaka miwili iliopita, pamoja na bei ya juu ya chakula na nishati, bei ambazo zilianza kuhujumu taifa hilo kuanzia mwaka jana. Wakati huo huo, kwa sababu ya upungufu wa misaada inayofadhiliwa WFP kuendesha operesheni zake, shirika limelazimika kupunguza ile posho ya chakula inayogawa kwenye mataifa muhitaji. Ofisi ya UM inayohusika na misaada ya dharura (OCHA), imeripoti idadi ya raia wa Ethiopia wanaohitajia msaada wa chakula imeongezeka, kuanzia mwezi Januari mwaka huu, kutoka watu muhitaji milioni 4.9 na hii leo jumla ya watu muhitaji imefikia milioni 6.2. Gharama za kuhudumia umma huu chakula, kayika kipindi cha baina ya miezi ya Oktoba mpaka Disemba 2009, zimekadiriwa kufikia dola milioni 175, mchango ambao bado haujapokewa kutoka wahisani wa kimataifa. Takwimu za Shirika la UM linashughulikia huduma za watoto, UNICEF, zimeonyesha vile vile watoto 250,000 wanakabiliwa na hali hatari ya utapiamlo katika Ethiopia na wanahitajia posho ziada kunusuru maisha.