Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika milioni sita ziada wa ukame Ethiopia wanahitajia misaada ya dharura ya chakula

Waathirika milioni sita ziada wa ukame Ethiopia wanahitajia misaada ya dharura ya chakula

Serikali ya Ethiopia na mashirika ya kimataifa yenye kuhusika na misaada ya kiutu yametangaza kunahitajika mchango wa dharura ziada wa dola miilioni 175 kwa mwaka huu, kuhudumia kihali watu milioni 6.2 walioathirika sana na mavuno haba na ukame wa muda mrefu uliosakama katika Ethiopia katika kipindi cha karibuni.

Tangu mwezi Januari 2009 idadi ya umma muhitaji kwenye eneo hili ulikuwa ukiongezeka kwa taratibu, wakati akiba ya chakula kwa ujumla nchini Ethiopia tangu hapo ilikuwa ni ya kigeugeu, kwa sababu ya mvua haba zilizonyesha 2008 ikichanganyika na bei yajuu ya chakula katika soko la kimataifa.