Skip to main content

Ofisa wa UNICEF anasema watoto wamedhurika zaidi na athari za mgogoro sugu wa JAK

Ofisa wa UNICEF anasema watoto wamedhurika zaidi na athari za mgogoro sugu wa JAK

Hilde Johnson, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), baada ya kuzuru Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK) ameeleza kwamba matatizo yaliolizonga taifa hilo huathiri pakubwa watoto wadogo, na hali hiihuenda ikaharibika zaidi pindi wahisani wa kimataifa watashindwa kuharakisha misaada inayohitajika kidharura kuhudumia kihali watoto hawa.

Matatizo yanayokabili JAK sasa hivi yanachochewa zaidi na usalama ulioregarega katika nchi, ikichanganyika na mporomoko wa bajeti la taifa, pamoja na upungufu wa misaada ya kutoka wahisani wa kimataifa. Kwa mujibu wa ripoti za UM, jumla ya watu wanaoathirika kidhahiri kimaisha, na kuathirika kusio dhahiri, kutokana na mgogoro ulioselelea katika JAK, inakadiriwa milioni moja ziada, kati ya idadi ya watu milioni 4 wanaoishi nchini humo.