Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufukuzaji wa raia baina ya Angola na JKK waongeza kasi, imehadharisha UM

Ufukuzaji wa raia baina ya Angola na JKK waongeza kasi, imehadharisha UM

OCHA imeripoti kwaamba katika kipindi cha miezi miwili iliopita, imeshuhudia muongezeko mkubwa wa idadi ya wahamiaji wa JKK wanaofukuzwa kutoka Angola, na kulazimishwa kuvuka mipaka kurejea makwao.

Tume maalumu ya mashirika yanayohudumia misaada ya kiutu, ikiongozwa na OCHA, ilipelekwa jimbo la Bas-Congo, mapema wiki hii, kutathminia hali, kwa ujumla. Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa kwa sasa, raia wahamiaji wa Angola, baina ya 20,000 mpaka 40,000 walikutikana wakiishi kwenye makazi ya muda yaliopo katika vituo vya mpakani vya Lufu na Kuzi, katika jimbo la Bas-Congo.