Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya waliong'olewa mastakimu Kivu Kaskazini waanza kurejea makwao, imetangaza OCHA

Maelfu ya waliong'olewa mastakimu Kivu Kaskazini waanza kurejea makwao, imetangaza OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeeleza kwamba katika miezi miwili iliopita, inakadiria watu 110,000 waliong\'olewa makazi na mapigano waliweza kurejea makwao katika jimbo la Kivu Kaskazini la JKK.

 Jamii nzima ya wahamiaji hawa muhitaji huwa inahudumiwa misaada ya kihali na mashirika ya UM, bila ya kubaguliwa. Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) linaendeleza shughuli za kugawa posho ya chakula kwa miezi mitatu ijayo, kwa wahamiaji wa Kivu Kaskazini, wakati Shirika linalohusika na Huduma za Wahamiji (UNHCR), kwa upande wake limeripotiwa kugawa misaada mengineyo ya kihali, na vile vile Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limewapatia umma huo vifaa vya kulimia pamoja na zana nyenginezo zinazohitajika kuendeleza kadhia hiyo. Hata hivyo, OCHA imeeleza kwamba watu 980,000 bado wamesalia bila ya makazi katika JKK na wanahitajia kufadhiliwa misaada ya kiutu na wahisani wa kimataifa.