Mkariri Huru wa Haki za Binadamu akaribishwa kuzuru Zimbabwe kwa mara ya awali
Manfred Nowak, Mkariri Maalumu Huru wa haki za binadamu, anayelenga shughuli zake kwenye masuala yanayohusu mateso, na adhabu nyengine katili zilizokiuka utu, ameripotiwa kuwa amepokea mwaliko rasmi kutoka Serikali ya Zimbabwe kulizuru taifa hilo la kusini mwa Afrika,
kuanzia tarehe 28 Oktoba mpaka Novemba 04, 2009 kuendeleza ukaguzi wa hali ya magereza na vizuizi vyenginevyo viliopo nchini na haki za wafungwa. Hii ni mara ya kwanza kwa Serikali ya Zimbabwe kuidhinisha wataalamu wanaohusika na mashirika ya UM yanayoshughulikia haki za binadamu kuzuru taifa lao. Nowak alieleza hatua hii, kwa ufahamivu wake, huashiria dalili ya kutia moyo yenye kuonyesha Serikali ya Zimbabwe sasa ipo tayari kujihusisha zaidi na Mifumo ya UM Kwenye Utekelezaji wa Haki za Binadamu.