Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Chakula Duniani

Siku ya Chakula Duniani

Siku ya leo inaadhmishwa na UM kama ni Siku ya Chakula Duniani. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) watu bilioni moja ziada wanasumbuliwa na njaa sugu ulimwenguni kwa sasa, na hawana uwezo wa kupata chakula.

Kwa hivyo, WFP imependekeza tuiite siku hiyo kama "Siku ya Kukosa Chakula" badala ya kuiadhimisha kama ni "Siku ya chakula Duniani". Hata hivyo, Mkurugensi Mkuu wa WFP, Josette Sheeran, alinakiliwa akipongeza mchango wa nchi wanachama katika kuhudumia misaada ya chakula kwa mataifa muhitaji, licha ya kuwa mataifa haya yanaendelea "kukabiliwa na matatizo ya kiuchumi kwenye maeneo yao."