Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu laidhinisha ripoti ya mashambulio ya Ghaza, na kuishtumu Israel kwa makosa ya vita

Baraza la Haki za Binadamu laidhinisha ripoti ya mashambulio ya Ghaza, na kuishtumu Israel kwa makosa ya vita

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu, leo limepitisha azimio la kuidhinisha ripoti ya Jaji Richard Goldstone ilioandaliwa na Tume ya Kuchunguza Ukweli juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza, ripoti ambayo ilituhumu vikosi vya Israel na wapambanaji wa KiFalastina kufanya makosa ya vita.