FAO inakhofia kunywea kwa Ziwa Chad huenda kukazusha maafa ya kiutu kieneo

15 Oktoba 2009

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti juu ya kunywea kwa mali ya asili ya maji katika Ziwa Chad, hali ambayo itaathiri uwezo wa watu milioni 30 wanaoishi karibui na eneo hilo kupata rizki.

FAO inaashiria Ziwa Chad huenda likakauka na kutoweka mnamo miongo miwili ijayo, kwa sababu ya athari zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa na shinikizo za kimaisha zinazotokanana shughuli za umma unaoishi kwenye sehemu hii ya Afrika ya Kati. Ziwa Chad limezungukwa na mataifa ya Cameroon, Chad, Niger na Nigeria, na eneo la ziwa ambalo, kuanzia 1963, limeshapungua kwa asilimia 90, ambapo eneo la maji la Ziwa Chad lilikuwa na kipimo cha kilomita za mraba 25,000, wakati katika 2001 eneo hilo hilo, lilinywea na kujumlisha kilomita za mraba 1,500 tu. Shirika la FAO limehadharisha pindi maji kwenye Ziwa Chad yataendelea kupungua, kwa kasi ya kiwango kilichoshuhudiwa miaka ya karibuni, na ikiwa jumuiya ya kimataifa itashindwa kuchukua hatua za dharura kuidhibiti hali hiyo, inaashiriwa Ziwa Chad litatoweka kabisa mnamo miaka 20 ijayo.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter