UNAMID imelaani shambulio la vikosi vyake katika Darfur

UNAMID imelaani shambulio la vikosi vyake katika Darfur

UM umepokea ripoti zenye kueleza mnamo Ijumatatu usiku, saa 3:45 majira ya Sudan, majambazi watatu, wasiotambuliwa, waliochukua bunduki, walifyatua risasi kwenye kituo cha ulinzi cha Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) katika eneo la Kutum, Darfur Kaskazini na kumjeruhi askari mlinziamani mmoja.