Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya Pamoja juu ya Usalama Usomali yakutana Nairobi na yahimizwa na Mjumbe wa KM kuendelea na majadiliano ya amani

Kamati ya Pamoja juu ya Usalama Usomali yakutana Nairobi na yahimizwa na Mjumbe wa KM kuendelea na majadiliano ya amani

Mjumbe Maalumu wa UM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah aliripotiwa kuzungumzia ufunguzi wa mashauriano wa ile Kamati ya Pamoja kuhusu Usalama Usomali, iliokutana Ijumatatu asubuhi kwenye mji wa Nairobi, Kenya.

Ould-Abdallah aliwasihi viongozi wa Usomali kuendelea kushirikiana, kwa mazungumzo, juu ya taratibu za kuchukuliwa, kwa pamoja, kutafuta utulivu na amani nchini mwao. Alitllia mkazo juu ya umuhimu wa kuhakikisha vikosi vya usalama vyenye ujuzi, na utaratibu unaoaminika, vitaweza kuanza kazi rasmi nchini katika 2011, wakati ambapo muda wa madaraka ya serikali ya mpito utakapomalizika. Kadhalika Ould-Abdallah aliwataka wawakilishi wa Jamii ya Kimataifa kulenga shughuli zao zaidi kwenye yale masuala yenye kuhusu usalama, ugawaji wa misaada ya kiutu kwa waathirika wa uhasama, utekelezaji wa haki za binadamu na katika huduma za maendeleo, hasa katika kuzalisua ajira. Halkadhalika, aliwapongeza wanajeshi wa Shirika la UA la AMISOM na kusifu ushujaa wao katika kukabili matatizo ya kuimarisha usalama na kurudisha utulivu na amani katika Usomali.