Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wa ILO/WFP umethibitisha ajira isio rasmi huzinyima nchi maskini natija za biashara ya soko la kimataifa

Utafiti wa ILO/WFP umethibitisha ajira isio rasmi huzinyima nchi maskini natija za biashara ya soko la kimataifa

Utafiti ulioendelezwa bia karibuni na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) na Shirika la Biashara Duniani (WTO) umegundua kuwa ajira kubwa isio rasmi hukutikana katika nchi zinazoendelea,

hali ambayo huwakosesha nchi hizi fursa ya kufaidika na biashara huru iliopamba sasa hivi kwenye soko la kimataifa, mazingira ambayo utafiti unasema huwanasa wafanyakazi wa sekta, isio rasmi, kwenye mtego wa ufukara pindi watataka kubadilisha vibarua hivyo. Utafiti ulilenga uchunguzi wake kwenye fungamano ziliopo baina ya ajira isio rasmi na shughuli za katika soko la kimataifa, na iligundua ajira, isio rasmi, imesambaa zaidi katika mataifa mengi yanayoendelea, hali ambayo huwanyima wafanyakazi hao dhamana ya kupatiwa kibarua cha muda mrefu, na huchuma pato dogo na wakati huo huo hukosa ruzuku ya jamii ambayo serikali, kawaida, huwapatia watu waliaojiriwa kwenye sekta rasmi ya uchumi pale wanapokuwa hawana kazi, kwa muda. Vibarua vya ajira isio rasmi hujumlisha shughuli za binafsi zisiosajiliwa na sheria za kitaifa, na ambazo hazitoi ruzuku za kijamii, na huwakilisha watu waliojiajiri binafsi au wale wanaojiriwa kutoka aila moja.