Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM amekaribisha hatua ya kuunda serikali ya mpito Bukini

KM amekaribisha hatua ya kuunda serikali ya mpito Bukini

Ofisi ya msemaji wa KM imeripoti Ban Ki-moon ameyakaribisha kidhati mafanikio ya karibuni nchini Bukini katika kuunda Serikali ya Muungano wa Taifa.

KM alitangaza taarifa iliowahimiza viongozi wa Bukini kujitahidi kukamilisha majadiliano yao juu ya uteuzi wa wawakilishi wa serikali ya mpito, na kujaribu kufanya makubaliano yanayoridhisha, yatakayohakikisha mfumo wa mpito unatekelezwa bila ya matatizo. UM, kwa upande wake, alisema utaendelea kujihusisha kwenye mpango wa upatanishi, kwa kupitia Timu ya Usuluhishi wa Pamoja kwa Bukini, inayoongozwa na Raisi mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano. Vile vile UM umetangaza ya kuwa utaendelea kuhakikisha Itifaki ya Maputo inahishimiwa na kutekelezwa kama inavyokusudiwa, kwa lengo la kurudisha haraka utaratibu wa kikatiba nchini, kwa kuitisha uchaguzi unaoaminika na kuridhiwa na makundi yote husika ya kisiasa.