Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Benki Kuu ya Dunia ameahidi mabadiliko yanayofaa kukabili mizozo mipya ulimwenguni

Mkuu wa Benki Kuu ya Dunia ameahidi mabadiliko yanayofaa kukabili mizozo mipya ulimwenguni

Mkutano wa mwaka wa Kundi la Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) unaofanyika wiki hii kwenye mji wa Istanbul, Uturuki unazingatia mizozo ya kiuchumi na kifedha iliokabili ulimwengu katika kipindi cha hivi sasa.

Kwenye hotuba ya ufunguzi, Raisi wa Benki Kuu ya Dunia, Robert Zoellick aliwaambia wajumbe wanachama waliohudhuria mkutano ya kuwa taasisi yake imo mbioni kufuatilia zile juhudi za kuleta mageuzi, ya hali ya juu, kwenye shughuli zake, mabadiliko ambayo, alisistiza, yataifanya Benki Kuu ya Dunia kuendeleza kazi zake kwa ufanisi wa kuridhisha katika yale mataifa husika. Aliahidi mabadiliko yatakayofanyika katika Benki Kuu ya Dunia yatalenga kwenye bidii za pamoja za kuimarisha miradi ya maendeleo, na katika kuendeleza uwajibikaji kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikichaganyika na utawala bora; na wakati huo huo kuhakikisha gharama zinazotumiwa kutekeleza miradi zinalingana na faida inayoletwa na mipango hiyo.