Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM aisihi jumuiya ya kimataifa kuisaidia Serikali ya TFG Usomali kusalia

KM aisihi jumuiya ya kimataifa kuisaidia Serikali ya TFG Usomali kusalia

Ripoti mpya ya KM juu ya hali katika Usomali, iliochapishwa hii leo, imeeleza kwamba licha ya kuwa Serikali ya Mpito (TFG) nchini humo, inaelekea iliokoka na matishio ya kupinduliwa na makundi ya wapinzani - makundi yaliopalilia mapigano katika kipindi cha karibuni - hata hivyo serikali bado inakabiliwa na vizingiti kadha wa kadha dhidi yake, hasa kwenye yale masuala yanayohusu usalama na utulivu wa kisiasa.