Skip to main content

Mataifa ya Bahari ya Hindi kushiriki kwenye mazoezi ya tahadhari za mapema dhidi ya dhoruba za tsunami

Mataifa ya Bahari ya Hindi kushiriki kwenye mazoezi ya tahadhari za mapema dhidi ya dhoruba za tsunami

UM umetangaza kwamba mnamo tarehe 14 Oktoba, nchi 18 ziliopo kwenye eneo linalojulikana kama Mzingo wa Bahari ya Hindi zitashiriki kwenye mazoezi ya tahadhari kinga dhidi ya ajali ya mawimbi ya tsunami.

Tarehe hiyo inafungamana na Siku ya Kupunguza Maafa Duniani. Mazoezi ya nchi za maeneo ya Mzingo wa Bahari ya Hindi yatahusika na majaribio ya zile zana za kuhadharisha mapema maafa, zilizoanza kutumiwa katika 2004, baada ya mawimbi makali ya tsunami kugharikisha vibaya maeneo hayo kuanzia Australia hadi Afrika Kusini. Kufuatia tukio hili, Shirika la UM juu ya Ilimu, Sayansi na Utanaduni (UNESCO), kwa kupitia Kamisheni ya Sayansi ya Bahari (IOC), lilizisaidia nchi ziliopo kwenye ukingo wa Bahari ya Hindi kupatiwa Mfumo Mpya wa Kutabiri Mapema Dhoruba za Tsunami katika Bahari ya Hindi (IOTWS). Mataifa yatakayoshiriki kwenye mazoezi haya yaliopo ukingoni mwa Bahari ya Hindi katika Afrika Mashariki yatajumlisha Kenya, Bukini. Mauritius, Msumbiji, Seychelles na Tanzania.