Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu limeakhirisha kupitisha azimio juu ya mashambulio ya katika Tarafa ya Ghaza

Baraza la Haki za Binadamu limeakhirisha kupitisha azimio juu ya mashambulio ya katika Tarafa ya Ghaza

Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu limeakhirisha kuidhinisha ile ripoti maalumu ya Tume ya Uchunguzi juu ya Mzozo wa Tarafa ya Ghaza.

Ripoti inayojulikana kama Ripoti ya Goldstone, ilieleza kwamba Israel na wapiganaji wa KiFalastina katika Ghaza walikutikana kufanya makosa ya vita wakati wa mapigano yaliotukia mwisho wa 2008 na mwanzo wa mwaka huu kwenye Tarafa ya Ghaza. Baraza lilitazamiwa kupiga kura azimio liliokuwa na lengo la kuilaani Israel kukataa kushirikiana na uchunguzi wa makosa ya vita ulioendelezwa na kiongozi wa Tume, Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini na ambaye ripoti yake sasa imetumiwa Baraza la Usalama. Mwakilishi wa Pakistan kwenye Baraza la Haki za Binadamu, Balozi Zamir Akram, akizungumzia kwa niaba ya mataifa yaliodhaminia azimio, ikijumuisha nchi za KiArabu, wajumeb wa Afrika na wawakilishi wanachama wa Shirika la Umoja wa Nchi za KiIslamu, aliomba rasmi kura ya azimio icheleweshwe mpaka kwenye kikao kijacho cha Baraza ambacho kinatazamiwa kukutanana mwezi Machi 2010.