Vietnam yachukua madaraka ya kuongoza Baraza la Usalama kwa Oktoba

2 Oktoba 2009

Kuanzia siku ya leo, Vietnam imekabidhiwa Uraisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba. Balozi wa Kudumu wa Vietnam katika UM, Le Luong Minh, sasa hivi anashauriana na wajumbe wa Baraza la Usalama juu ya ratiba ya mwezi huu kuhusu shughuli zao.

Ajenda kamili ya Baraza la Usalama kwa mwezi Oktoba inatazamiwa kutangazwa rasmi Ijumaa ya kesho.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter