UNAMID imekamilisha thuluthi mbili ya maofisa wa polisi wanaohitajika kulinda raia

UNAMID imekamilisha thuluthi mbili ya maofisa wa polisi wanaohitajika kulinda raia

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) leo limeripoti kuwasili kwenye mji wa El Fasher, wiki hii, maofisa wa polisi 130 watakaotumiwa kuimarisha usalama kwenye kambi za wahamiaji wa ndani ya nchi.

Jumla ya vikosi vya polisi wa kimataifa katika Darfur kwa hivi sasa ni polisi 1,675, ikijumuisha asilimia 65 ya idadi ya polisi wanaotakiwa kuenezwa kwenye maeneo yenye mvutano katika Darfur ili kulinda na kuhifadhi raia.