Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame katika Uganda unaitia wasiwasi WFP

Ukame katika Uganda unaitia wasiwasi WFP

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti rasmi hii leo kuingiwa wasiwasi kuhusu mfululizo wa mvua haba katika Uganda kwenye majira ya mvua, hali iliosababisha watu milioni mbili kukosa uwezo wa kupata chakula na kuomba wasaidiwe chakula na mashirika ya kimataifa kunusuru maisha.

Katika jimbo la kaskazini-mashariki la Karamoja, hali huko inaripotiwa kuwa ni mbaya sana, na WFP imelazimika kwa sasa kushirkiana na serikali kuongeza operesheni za kugawa chakula kwa watu muhitaji ziada milioni 1.1, idadi ambayo inajumlisha asilimia 90 ya wakazi wa eneo. Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Josette Sheeran ametangaza Ijumanne taarifa maalumu yenye kutilia mkazo wajibu wa UM kuupatia umma wa eneo husika msaada wa chakula kwa sababu wameghumiwa na kusumbuliwa na utapiamlo mbaya na hatari, wa mara kwa mara, ukichanganyika na njaa sugu. Hata hivyo, Sheeran alisema WFP italazimika kupunguza posho ya chakula inayogawa kwenye operesheni zake nchini Uganda, kama ilivyofanya mwezi Aprili, kwa sababu ya upungufu wa mchango wa fedha kutoka wahisani wa kimataifa, fedha ambazo zinahitajika kuhudumia operesheni zao kieneo. Alisema mchango wa dola milioni 66 unatakikana, hivi sasa, kwa WFP kuweza kuendeleza operesheni zake, kamainavyostahili, katika Karamoja, kwa miezi sita ijayo.