Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matayarisho ya mkutano wa Copenhagen yanavuta kasi Bangkok

Matayarisho ya mkutano wa Copenhagen yanavuta kasi Bangkok

Wajumbe wa kimataifa wanaokutana kwa sasa mjini Bangkok, Thailand Ijumatatu walianzisha majadiliano yanayokaribia duru ya mwisho ya maandalizi ya mkutano mkuu ujao wa Copenhagen,

mkutano unaotarajiwa kuzingatia udhibiti wa pamoja wa athari zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni, kikao ambacho wawakilishi wa kutoka wananchi wanachama wanatarajiwa kuwasilisha mkataba mpya wa kuritihi maafikiano ya Mkataba wa Kyoto. Waziri Mkuu wa Thailand, Abhisiti Vejjajiva alisema kwenye risala yake mkutanoni kwamba ridhaa ya kisiasa na mawazo yaliokubaliwa na viongozi wa kimataifa, walipokutana hapa Makao Makuu wiki iliopita, yatatumiwa kuwaongoza wajumbe waliohudhuria kikao cha Bangkok, kukamilisha, kwa mfanikio, itifaki yao kabla ya mkusanyiko wa Copenhagen. Alikumbusha kwamba kiliopo sasa ni mradi mmoja tu unaohitajia kupitishwa kimataifa, nao ni ule mpango aliouita "mradi wa A", yaani mradi wa nambari moja pekee; na alisisitiza hakuna tena mradi wa nambari ya pili, alioufananisha na mradi wa B. Alionya kwamba walimwengu wakishindwa kufikia mapatano ya mradi wa A, watabakiza "mradi wa F" - ambao aliufananisha na hali ya kushindwa kulikotota, kufeli na kutofaulu kwenye kadhia ya kuimarisha maendelo ya kudhibiti bora taathira za mabadiliko ya hali ya hewa katika dunia.