Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Usomali wanaelekea Kenya kunusuru maisha kufuata mapigano na ukame nchini mwao: UNHCR

Raia wa Usomali wanaelekea Kenya kunusuru maisha kufuata mapigano na ukame nchini mwao: UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba tangu mwanzo wa mwaka raia wa Usomali 50,000 ziada wamehamia Kenya kutafuta hifadhi ya maisha.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR wahamiaji 6,400 huwasili Kenya kila mwezi, hali ambayo inaweka shinikizo zaidi kwenye huduma za kihali katika kambi iliofurika watu ya Dadaab. UNHCR ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) yamefanikiwa sasa hivi kuwahamisha wakazi 9,500 kutoka kambi ya Dadaab na kuwapeleka kwenye eneo la Kakuma, kaskazini-magharibi nchini Kenya ili kupunguza msongamano wa makazi kwa wahamiaji wa Usomali. UNHCR imeripoti kwamba Wasomali 250,000 walilazimika kuhama makazi yao baada ya mapigano kushtadi kwenye mji mkuu wa Mogadishu, kuanzia mwezi Mei, baina ya vikosi vya serikali na majeshi ya mgambo ya wapinzani. Wingi wa wahamiaji hawa walikimbilia ushoroba wa Afgooye, kilomita 30 kutoka Mogadishu kutafuta hifadhi.