Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA inaadhimisha miaka 60

UNRWA inaadhimisha miaka 60

Viongozi wa kitaifa na mawaziri wa vyeo vya juu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikusanyika leo hii kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York kuhishimu mchango wa Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) kuhudumia kihali umma wa KiFalastina, shirika ambalo leo limetimiza miaka 60 tangu kubuniwa.