Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya wahusika wengi ndio inayohitajika kutatua mizozo ya kimataifa, asihi Raisi wa BK

Suluhu ya wahusika wengi ndio inayohitajika kutatua mizozo ya kimataifa, asihi Raisi wa BK

Raisi wa Baraza Kuu (BK), Ali Treiki wa Libya, kwenye risala yake ya ufunguzi wa majadiliano ya jumla, aliyahimiza Mataifa Wanachama kushirikiana, kwa ukaribu zaidi, na taasisi ya UM.

Alisisitiza ya kuwa utaratibu wenye mafanikio ya kuitatua mizozo mikuu ya kimataifa ni ule wenye wahusika wengi, na UM ndio jukwaa halali, lenye uwezo wa kuhakikisha kunachukuliwa hatua zinazoridhisha kimataifa. Alisema mizozo iliyogawanyika, yenye sehemu nyingi - inayojumuisha mabadiliko ya hali ya hewa, upunguzaji wa silaha, ufukara uliopita kiasi, majanga ya UKIMWI na VVU, na migogoro ya chakula na nishati - ni masuala yenye kuthibitisha, wazi kabisa, ulazima wa kuwa na ushirikiano wa hali ya juu miongoni mwa nchi wanachama ili kusuluhisha mizozo ya kimataifa.