Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa taasisi ya ICGLR azungumza na Redio ya UM juu ya shughuli za shirika lao

Mkurugenzi wa taasisi ya ICGLR azungumza na Redio ya UM juu ya shughuli za shirika lao

Siku ya leo, Ijumatatu tarehe 21 Septemba, ofisi za UM za Makao Makuu zimefungwa rasmi kwa sababu ya Siku Kuu ya Eid al Fitr. Kwa hivyo, badala ya taarifa za habari za kila siku, leo tumekuandalieni kipindi maalumu kuhusu shughuli za Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGRL) yenye makao yake rasmi mjini Bujumbura, Burundi. Makala hii itaongozwa na mimi AWK.

Hivi karibuni, mfanyakazi mwenzetu anayetayarisha vipindi vya Kifaransa wa Redio ya UM, Jean-Pierre Ramazani, mzalia wa JKK, alizuru eneo la Maziwa Makuu. Alipokuwepo huko alikutana na kufanya mahojiano na watu mbalimbali kuhusu masuala ya usalama, amani, maendeleo ya kiuchumi na jamii na kadhalika. Alipokuwa Burundi, Ramazani alifanya mahojiano na Balozi Liberata Mulamula, mkuu wa Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Kanda ya Maziwa Makuu.

Sikiliza mazungumzo hayo kwenye idhaa ya mtandao.