Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamishna wa Haki za Binadamu ashtushwa na shambulio la kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani Yemen

Kamishna wa Haki za Binadamu ashtushwa na shambulio la kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani Yemen

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu Ijumaa ilioleza kusumbuliwa sana na taarifa za watu walioshuhudia shambulio la ndege za Yemen, liliotukia tarehe 16 Septemba, kwenye kambi ya muda ya raia waliokimbia mapigano baina ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Al Houthi, tukio ambalo limesababisha darzeni kadha za vifo vya wahamiaji hawo wa ndani ya nchi.

Bi Pillay aliomba serikali ya yemen kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za haraka kuhakikisha kitendo hiki hakitorudiwa tena. Alisema hali ya mzozo uliotapakaa katika Yemen kaskazini ni ya wasiwasi kutokana na athari zake mbaya kwa usalama wa raia. Aliikumbusha serikali ya Yemen pamoja na majeshi ya taifa juu ya dhamana yao ya kulinda na kuwahifadhi raia walionaswa kwenye mazingira ya mapigano, kwa kulingana na sheria za kiutu za kimataifa na sheria za haki za kibinadamu.