Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale

Hapa na pale

Ofisi ya UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) imetangaza kushtushwa sana na kutishwa na idadi ya vifo vilivyosajiliwa katika eneo la uhasama la Yemen. UNHCR imeshapeleka mahema zaidi, magodoro na mablangeti kwa wahamiaji 2,000 ziada waliomiminikia kwenye eneo jirani la Saudi Arabia kutafuta hifadhi. Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya taarifa ilizopokea zinazosema mashambulio ya anga yaliofanyika karibuni kwenye kambi za wahamiaji wa ndani katika Yemen kaskazini, yalisababisha vifo kadha vya raia, ikijumlisha watoto wadogo. UNICEF ilisema hali hiyo ni msiba mkubwa katika Yemen kaskazini, hususan kwa watoto wadogo ambao mwezi mmoja tangu mapigano kufumka bado hawana fursa ya kupatiwa maji safi na salama, wala mazingira yanayoridhisha au utunzaji wa afya na hifadhi wanayostahiki.

Baraza la Usalama asubuhi liliitisha mkutano wa hadhara juu ya hali katika Mashariki ya Kati ambao ulifuatiwa na kikao cha faragha. Robert Serry, Mratibu Maalumu wa KM juu ya Mpango wa Amani Mashariki ya Kati alisema kwenye hotuba yake mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba wanaoshika mamlaka wa KiFalastina hivi sasa ni "washirika imara wa amani". Aliwafananisha na watendaji walio tayari kutekeleza majukumu yao, wanaosisitiza haki zao halali za kiutu ni lazima kuhishimiwa, lakini alisema kilichopungua kwa sasa, alitilia mkazo, ni ukosefu wa mchango wa taifa liliokalia maeneo ya WaFalastina la Israel, pamoja na msaada wa kutoka mataifa ya kieneo na mchango wa walimwengu, mchango unaohitajika kuwawezesha wenye mamlaka wa KiFalastina kutekeleza shughuli zao za utawala kama inavyotakiwa. Juu ya hali katika Tarafa ya Ghaza, Serry alisema "hali hiyo haiwezi kuruhusiwa kuendelea kama ilivyo sasa hivi, kwa sababu inawakilisha mazingira hatari na haiwakilishi hata kidogo masilahi ya wale wote wanaohusika na mzozo wa Ghaza". Alisema KM aliitumia Israel, mnamo mwezi Juni, ombi la kutaka kuruhusiwa kuingizwa Ghaza vifaa vya ujenzi wa majengo ya kiraia. Lakini KM bado bado anasubiri jawabu kutoka kwa watawala hawo hadi hivi sasa.